Yakiwa yamebaki lisaa 1 tu dunia isimame kwa muda wa lisaa 1 na nusu kupisha tukio la kihistoria ambalo linatokea pale kiyv usiku wa leo majira ya saa 3 usiku kwenye mchezo wa fainali baina ya miamba yenye historia kubwa katika mashindano haya Real madrid pia mabingwa watetezi kwa miaka miwili mfululizo dhidi ya Liverpool ambao ni mabigwa wa mara 5 pia katika mashindano haya.
Mara ya mwisho liverpool walichukua ubingwa mbele ya ac millan wakitoka nyuma kwa goli 3 mpaka ubingwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati mwaka 2005. Na walicheza tena fainali yao ya mwisho mwaka 2007 dhidi ya ac millan na walifungwa katika mchezo huo.
kuelekea mchezo huu timu hizi zimekutana mara 6 katika mashindano ya ulaya liverpool akiwa na rekodi nzuri mbele ya madrid ,akiwa ameshinda michezo 3 na Real madrid akiwa ameshinda michezo 2 huku sare mchezo mmoja.
katika michezo hiyo liverpool amefunga mabao 6 huku madrid akiwa amefunga magoli 4 .
liverpool wamekuwa na msimu nzuri mwaka huu huku nyota wake watatu mo salah, mane na firmino wakiwa bora zaidi ya safu yoyote katika mashindano haya wakiwa tayari wamefunga mabao 29 peke yao.
Mo salah na Ronaldo watu wengi wanakwenda kuwaangalia hawa kila mmoja atafanya nini kwa timu yake ukilinganisha watu wengi wanasema mo salah ni bora zaidi duniani kwa sasa kuliko mchezaji yoyote ndani ya msimu huu kulingana na rekodi amabazo ameziweka.
Lakini madrid wanakuwa watofauti sana wanapofika katika fainali hasa za mashindano haya. kocha wa madrid zidane ameingia fainali 6 na zote ameshinda toka amekuwa kocha wa Real madrid.
Je karata yako unampa nani?
tuachie maoni yako hapo chini sehemu ya comment.
No comments:
Post a Comment