WAJUE NYOTA WALIOACHWA NA SIMBA KUELEKEA MCHEZO WAKE NA MAJIMAJI FC - EDUSPORTSTZ

Latest

WAJUE NYOTA WALIOACHWA NA SIMBA KUELEKEA MCHEZO WAKE NA MAJIMAJI FC


wachezaji wa simba na yanga wakisakata kabumbu
WAJUE NYOTA WALIOACHWA NA SIMBA KUELEKEA MCHEZO WAKE NA MAJIMAJI FC

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu huu, wameondoka bila wachezaji baadhi waliocheza mchezo  wa ligi ambao walikabidhiwa kombe dhidi ya Kagera Sugar kwa ajili ya kuwapumzisha.

Nyota John Bocco, Shiza Kichuya na Emmanuel Okwi ni miongoni mwa wachezaji waliosalia Dar es Salaam huku wengi wa kikosi cha pili wakisafiri na timu kuhitimisha safari ya msimu huu.

Wachezaji hao wameamua kupumzishwa kwa ajili ya maandalizi ya baadaye ya SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza mwezi Juni 2018 nchini Kenya.

Kuelekea mechi hiyo, uongozi Simba umesema hawaendi kuihurumia Majimaji bali wanaenda kuweka heshima ya kupigania matokeo.

Mtoa taarifa huyo alisema msafara huo unatarajiwa kuwa na wachezaji 17 pekee pamoja na benchi la ufundi.

“Katika msafara wetu wachezaji ambao wakongwe watakaosafiri ni Niyonzima (Haruna), Mzamiru (Yasin) na Ndemla (Said) pekee, wengine waliobaki watakuwa ni vijana wa U20.

“Akina Bocco, Okwi na Kichuya (Shiza), Kwasi (Asante) na wengine waliotumika katika kikosi cha kwanza, wote watabaki kwa ajili ya mapumziko,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa timu hiyo, Said Tulliy kuzungumzia hilo, alisema kuwa “Ni kweli timu inasafiri kesho (leo) Jumamosi asubuhi kuelekea Songea kwa ajili ya mechi na Majimaji, lakini kuhusu kikosi kitakachokwenda benchi la ufundi ndio linajua.”

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz