TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA - EDUSPORTSTZ

Latest

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA

mpira wa miguu
Manchester United watatoa Euro milioni 140 kwa Real Madrid kumpata Gareth Bale
Manchester United watatoa Euro milioni 140m kwa Real Madrid kumnunua mchezaji wa safu ya kati Gareth Bale mwenye umri wa miaka 28 kutoka Wales. (AS)

Manchester United na Chelsea wameonesha nia ya kutaka kumsajili Mhispania Jordi Alba mwenye umri wa miaka 29 anayeichezea Barcelona. (Sport)

Rais wa klabu inayocheza ligi ya daraja la tatu nchini Italia Rimini FC amesema yuko tayari kumchukua mlinda lango wa Liverpool Loris Karius kwa mkopo wa mwaka mzima kama zawadi yake ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ambayo ni tarehe 22 Juni. Kwa hiyo Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 24 anaweza walau "kutulia na kujiamini tena" baada ya aibu aliyoipata katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. (Rimini FC)
West Ham wanafanya mazungumzo na Barcelona kwa malengo ya kusaini mkataba na Mbrazili anayecheza safu ya kati- kushoto - Marlon Santos mwenye umri wa miaka 22. (Mundo Deportivo)

Williams: Nilijihisi kama shujaa kutoka Wakanda
The Hammers pia wako makini kumleta mchezaji wa safu ya ulinzi wa Genoa Mwitaliano - Armando Izzo mwenye umri wa miaka 26- katika klabu hiyo. (Sky Sports)

Real Madrid ndio wenye fursa zaidi ya Arsenal ya kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya ulinzi wa Atletico Madrid, raia wa Uruguay Jose Gimenez, na wanatarajia kutimiza malipo yake mapya ya pauni milioni £53m . (Talksport)
Tottenham wana wasi wasi kwamba nia yao ya kumnunua Fulham Ryan itavurugwa na Shahid Khan
Inter Milan watatakiwa kulipa euro milioni 40 kumchukua mchezaji wa kiungo cha kati wa Barcelona Rafinha, mwenye umri wa miaka 25 raia wa Brazil ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu hiyo ya ligi kuu ya Italia katika msimu uliopita. (La Gazzetta dello Sport)

Vijana 11 wa Tanzania walioshtakiwa ubakaji Afrika Kusini waachiwa huru
Rais wa Lazio Claudio Lotito amesema kuwa alikataa kupokea euro milioni 110m (£95.75m) ili amuuze Mserbia Sergej Milinkovic-Savic mwenye umri wa miaka 23 anayecheza katika safu ya kati. (Football Italia)

Tottenham wana wasiwasi kuwa matumaini yao ya kusaini mkataba na Mwingereza anayechezea Fulham Ryan Sessegnon mwenye umri wa miaka 18 yatavurugwa na azma ya mmiliki wa mmiliki wa Fulham Shahid Khan ya kununua uwanja wa Wembley. (Evening Standard)

Manchester City imetangaza kuwa haina mpango wa kumuuza Phil Foden anayewachezea safu ya kati ambaye alitimiza umri wa miaka 18 Jumatatu.
Wakati huo huo, Spurs wanamfuatilia kwa karibu mlinda lango wa klabu ya Southampton Mwingereza Alex McCarthy, mwenye umri wa miaka 28. (Mirror)

Mchezaji wa Manchester City anayecheza katika safu ya kati Muingereza Phil Foden, ambaye alitimiza umri wa miaka 18 Jumatatu , atapewa mkataba mpya na hatauzwa kwa mkopo msimu ujao. (Telegraph)

Newcastle wanamtaka sana Fulham Ryan Fredericks
Mshambuliaji wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 26 Mnorway Joshua King anasema kuwa hafurahii namna meneja Eddie Howe alivyomtumia msimu uliopita. (VG via Independent)

Kipa wa Liverpool Loris Karius ashauriwa ahame
Newcastle wanataka kusaini mkataba na mlinzi wa Fulham Mwingereza Ryan Fredericks. (Newcastle Chronicle)

Mshambuliaji wa timu ya Leeds United raia wa Sweden Marcus Antonsson, mwenye umri wa miaka 27, hana uhakika wa hali yake ya baadae katika klabu hiyo inayocheza ligi ya Championship Uingereza. (Fotboll Direkt via Yorkshire Evening Post)


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz