MSIMAMO WA WACHEZAJI WA UINGEREZA KUHUSU UBAGUZI WA RANGI WAKATI WA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA - EDUSPORTSTZ

Latest

MSIMAMO WA WACHEZAJI WA UINGEREZA KUHUSU UBAGUZI WA RANGI WAKATI WA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA

Kombe

Wachezaji wa Uingereza wamezungumzia kuhusu hatua watakazochukua iwapo wenzao watabaguliwa kwa vigezo vya rangi katika michuano ya kombe la dunia nchini Urusi mwezi Juni kulingana na Ashley Young.

Shirikisho la soka nchini Urusi hivi majuzi lilipigwa faini ya £22,000 kwa kelele za ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Ufaransa mnamo mwezi Machi.

"Wakati unapokuwa katika uwanja hujui utakachofanya'' , alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32.

''Tumezungumza kuhusu swala hilo na tumelizungumzia katika kikosi chetu-kile tutakachofanya na kile ambacho hatutafanya''.

Kipa wa Liverpool Loris Karius ashauriwa ahame
Raheem Sterling akemewa kwa kuchora tatuu ya bunduki mguuni
Everton kumpa mkataba meneja wa zamani wa Watford Marco Silva
Aliongezea: Tuna matumaini Fifa itaweza kukabiliana na swala hilo.

Mchezaji wa Ufaransa Paul Pogba , Ousmane Dembele na Ngolo Kante walidaiwa kuwa miongoni mwa wachezaji walionyanyaswa katika mechi yao ya ushindi wa 3-1 dhidi ya waandalizi hao wa kombe la dunia.

Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Krestovsky mjini St Petersburg, ikiwa ni miongoni mwa viwanja vitakavyoandaa kombe hilo la dunia.

Taarifa kutoka kwa shirikisho la soka duniani Fifa imesema kuwa shirika hilo halitavumilia ubaguzi wowote.

Hatahivyo, Lord Ouseley , mwenyekiti wa kampeni dhidi ya ubaguzi wa rangi Kick It Out, aliitaja faini hiyo iliotolewa na Fifa kuwa hafifu mno.

'Wachezaji huwakasirisha ama kuwafurahisha watu'

Mchezaji huyo wa Manchester United alihusika katika mgogoro na mchezaji wa timu pinzani aliyeko katika kikosi cha Uingereza Dele Alli wakati timu zao zilipomenyana mwezi Oktoba.

United iliibuka na ushindi wa 1-0 na ijapokuwa Young anasema kuwa wawili hao wamefanya mzaha katika vikosi vya awali , anajua kwamba wachezaji wa Uingereza lazima wawe na tahadhari ya kuchokozwa nchini Urusi.

''Unajua katika uwanja wachezaji huwafurahisha ama hata kuwakasirisha mashabiki'', alisema. ''Hujaribu kuwalenga watu fulani. hutokea katika soka ya vilabu''

"Ni miongoni mwa maswala nyeti lakini lazima tuwe na wachezaji 11 uwanjani kila mara na nadhani kuna uzoefu wa kutosha katika kikosi hiki kujua iwapo mtu anachokozwa ili kuwaondoa na kuwaambia kuwa mtulivu ama hata kuzungumza na refa ili kumjulisha kinachoendelea''.

"Tumezungumza kuhusu visa tofauti. Hayo ni siri yetu lakini ninahakika kuna mambo yatafanyika katika mchuano huu''.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz