YANGA YAZIDI KUPASUA MIPAKA LICHA YA KUPOKEA KICHAPO CHA 1-0 KUTOKA KWA DICHA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 18 April 2018

YANGA YAZIDI KUPASUA MIPAKA LICHA YA KUPOKEA KICHAPO CHA 1-0 KUTOKA KWA DICHA

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuingia hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 2-1, licha ya kufungwa katika mchezo wa leo jioni na wapinzani wao Welayta Dicha.

Katika mchezo wa marudio uliochezwa Leo Yanga imethibitiwa kwa bao 1-0 kwenye mchezo uliomalizika jioni hii huko Ethiopia .
Licha ya klab ya yanga kufungwa, imesonga mbele kutokana na ushindi wa mabao 2-0 iliopata nyumbani kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam.

Hii sio mara ya kwanza kwa Yanga kutinga hatua ya makundi ambapo msimu wa 2015/16 iliingia katika hatua hiyo lakini ilimaliza katika nafasi ya mwisho na kushindwa kuendelea na michuano.

Yanga leo imecheza bila ya kocha wake mkuu George Lwandamina ambaye ameondoka klabuni hapo wiki iliyopita na kurejea kwenye timu yake ya zamani ya Zesco United ya Zambia.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment