SABABU ZINAZOPELEKEA KUWEPO KWA MICHEPUKO KATIKA MAHUSIANO - EDUSPORTSTZ

Latest

SABABU ZINAZOPELEKEA KUWEPO KWA MICHEPUKO KATIKA MAHUSIANO



Image result for lovers
Niliwahi kusema ya kwamba ya kwamba “mchepuko ni dili feki” wengi wakabishana sana, na leo naomba kurudia kusema ya kwamba mchepuko ni dili feki kwa sababu michepuko ndio chanzo cha mifarakano ya ndoa zilizo nyingi ulimwenguni kote hii ni kwa mujibu wa utafiti usio rasmi lakini ndio ukweli wenyewe. Na miongoni mwa sababu inayopelekea kutokea kwa michepuko ni:


Penzi kupoa au kufa
Penzi linapopoa au hata linapokufa huwa inaonyesha wazi kabisa dalili zote za awali. Kwenye kupoa mhusika anaweza kuanza kujihisi ndani ya moyo wake kutompenda mwenzake kama alivyokuwa akimpenda awali. Inawezekana mwenzake hajagundua kuanzia mwanzoni kwamba penzi la mpenzi wake limepoa ila kama hali ya kupoa huku itaendelea lazima itagundulika.

Baadhi ya vitu dhahiri vitakavyoweza kukufanya ufahamu kwamba penzi la mwenzako limepoa au kufa nikwamba kuna mambo ambayo uliyazoea kuyaona yakifanywa kawaida hautayaona tena. Kuna vitu vilikuwa vikifanywa pasipo kukumbushana sasa utalazimika kuviomba ili ufanyiwe, utaona kila kitu kinakuwa kigumu kumhusu mwenzako na hata uongeaji au kujibu kwake kunakuwa na walakini.

Kwenye tendo la ndoa nako maranyingi ndiko kwenye kuonyesha taa nyekundu mapema, ule ushiriki, furaha na bashasha zilizokuwapo awali mkiwa kwenye tendo hauzioni tena, tendo la ndoa linafanywa kama jukumu la kawaida na mara nyingine hata hamu ya kushiriki haipo. Hapa ndipo mmoja hukinai hiyo hali ya kulazimishana tendo la ndoa, au kupeana kwa masharti au kunyimwa au hata mmoja kupoteza hamasa ya kulifanya tendo hilo na mtu asiyekuwa na hisia naye.

Huo unakuwa mwanzo wa mmoja au wote kutoka nje ya mahusiano au ndoa. Penzi ni kama moto, ukiwashwa pasipo kuchochewa hupoa au hata kuzima kabisa. Wengi wanapoingia kwenye ndoa wanadhani mkishaoana basi mambo yanajiseti yenyewe tu, mapenzi yanajichanulia yenyewe tu, la hasha! Lazima kuwepo na jitihada za dhati za wanandoa kuhakikisha wanachochea penzi lao, kulilinda na kulipalilia ili liendelee kumea, kunawiri na kuzaaa matunda.

hivyo kupoa kwa penzi husababisha michepuko, hivyo ili uweze kuepuka jambo hili ni vyema ukaepuka visababishi vya ambavyo nimekwusha vieleza hapo awali.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz