MWAKYEMBE AMFUTIA ADHABU ROMA KWA SHARTI HILI - EDUSPORTSTZ

Latest

MWAKYEMBE AMFUTIA ADHABU ROMA KWA SHARTI HILI
Wizara ya Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni imemfutia adhabu Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo Roma Mkatoliki iliyokuwa imempatia kutokana na wimbo wake wa Kiba 100 kukosa maadili.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jioni, Waziri Mwakyembe amesema kwamba Wizara imeamua kumfungulia msanii huyo baada ya kukiri kuwa amefanya makosa na kuahidi kwamba atakuwa balozi wa maadili.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa msamaha wa msanii huyo utaanza mara moja pale ambapo msanii huyo atakapo kamilisha sharti la kujisajili kwenye Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) huku ikiwa hajapewa muda maalumu wa kukamilisha sharti hili.

"Sisi kama wizara tumepokea maombi ya Msanii Roma na niseme Mimi kama Waziri na kwa niaba ya Naibu Waziri tumemfutia adhabu Roma Mkatoliki lakini siku atakapokabidhiwa Cheti cha Usajii cha BASATA ndo siku adhabu yake itakapokuwa imekwisha" Mwakyembe.

Ameongeeza "Hatumpangii iwe lini akiweza afanye leo jioni kesho, baada ya Pasaka mwakani ni yeye, lakini siku atakapopata Cheti ndipo ataweza kuendelea na kazi zake na tunamtakia kila la kheri".

Kwa upande wa msanii Roma yeye ametoa tamko kwa mamlaka inayosimamia kazi za sanaa iweze kutoa wimbo huo katika vyombo vyote vya habari akimaanisha kuwa hataweza kuufanyia tena marekebisho yoyote kama jinsi ambavyo ilitakiwa awali.

Mwanzoni mwa mwezi Machi serikali kupitia Wizara ya Habari ilitangaza kumfungia miezi sita msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na masuala ya muziki kwa kukaidi amri ya kubadilisha baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa Kiba100.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz