YANGA YAFUNGUKA KUHUSU KAMSOKO NA NGOMA KUELEKEA MCHEZO WA JUMAMOSI - EDUSPORTSTZ

Latest

YANGA YAFUNGUKA KUHUSU KAMSOKO NA NGOMA KUELEKEA MCHEZO WA JUMAMOSI
Klabu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inatarajiwa kusafiri kesho kuelekea Mkoani Singida wakiwa wanatokea Morogoro kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Singida United mnamo Aprili mosi mchezo wao wa kombe la Shirikisho.

Hayo yamethibitishwa na Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh leo (Machi 29, 2018) na kusema programu ya mazoezi katika kambi ya timu hiyo iliyopo Morogoro inakamilika kesho asubuhi (Ijumaa) na baada ya mazoezi wataanza safari rasmi ya kuwafuata wapinzani wao.

"Kambi inaendelea vizuri, tunatarajia kuhitimisha mazoezi yetu siku ya Ijumaa asubuhi kisha timu itasafiri kuelekea Mkoani Singida tayari kwa mchezo. Donald Ngoma na Kamusoko wanaendelea vizuri na mazoezi kwa kufuata maelekezo ya mwalimu pamoja na benchi la ufundi kwa ujumla",amesema Saleh.

Kwa upande mwingine, Meneja Saleh amesema wachezaji wote kiujumla wanaendelea vizuri na wapo teyari kwa mchezo wao dhidi ya wapinzani wao Singida United utakaochezwa katika dimba la Namfua katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz