VIDEO: ALICHOKISEMA MKUU WA CHUO NIT KUHUSU KUAWA KWA AKWILINA - EDUSPORTSTZ

Latest

VIDEO: ALICHOKISEMA MKUU WA CHUO NIT KUHUSU KUAWA KWA AKWILINAChuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kimesema aliyepigwa risasi jana Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam na kufariki dunia ni mwanafunzi wa chuo hicho.

Chuo hicho kimemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Akwilina Akwiline aliyekuwa anasoma shahada ya kwanza ya ununuzi na ugavi.

Leo, Februari 17, 2018, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandamana jana.

Wafuasi hao wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe waliandamana kuelelea ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho.

Ofisa Uhusiano wa NIT, Ngasekela David amesema wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha wanafunzi huyo.

"Ni kweli alikuwa wanafunzi wetu na tumepokea kwa masikitiko taarifa hizi. Tunaendelea kufuatilia zaidi, "amesema David.


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au
kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.


Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz