SOMA ALICHOPOST MSIGWA KUHUSU TUHUMA ZA KUWA NA MASILAHI KATIKA MAKAMPUNI YA UWINDAJI - EDUSPORTSTZ

Latest

SOMA ALICHOPOST MSIGWA KUHUSU TUHUMA ZA KUWA NA MASILAHI KATIKA MAKAMPUNI YA UWINDAJI

Image result for peter msigwa
Peter Msigwa Amvaa Kigwangala Amtaka Atoe Ushahidi "Nipo Tayari Kujiuzulu Nafasi Yangu ya Ubunge"

Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kuweka wazi kuwa endapo Waziri wa Maliasili na Utalii atatoa ushahidi wowote ambao unaonyesha yeye ana masilahi na makampuni ya uwindaji atajiuzulu nafasi yake ya ubunge.

Mchungaji Msigwa amesema hayo Februari 12, 2018 kupitia moja ya mitandao yake ya kijamii na kudai kuwa Waziri huyo amekuwa ni muongo na ni mtu ambaye hajiamini

"Kigwangalah ni muongo anyependa masifa, ni mtu asiyejiamini. Kama akitoa ushahidi wowote utakaodhihirisha kuwa nina masilahi na makampuni ya uwindaji nitajiuzulu ubunge .Nina wasiwasi na upbringing yake" aliandika Msigwa

Mbunge Msigwa amesema hayo kufuatia kauli ambayo Waziri Kigwangalla aliitoa siku chache zilizopita kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa Mbunge huyo wa Iringa Mjini anahusika na ana hisa katika vitalu, jambo ambalo Msigwa mwenyewe amelipinga vikali na kuamua kuweka ubunge wake rehani endapo Waziri huyo atathibitisha hilo.

Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz