BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 13 February 2018

ALICHOKIPOSTI ZITTO KUHUSU MBWANA SAMTTAKiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe jana Februari 12, 2018 alikwenda kumtembelea Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta nyumbani kwake huko Genk nchini Ubelgiji.

Kabla ya kumtembelea Samatta, Zitto alifanikiwa pia kumtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu anayeendelea na matibabu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, nchini humo kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na risasi zaidi ya 36 na watu wasiojulikana, Septemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake eneo la Area D, Dodoma.

 Kupitia ukurasa wake wa twitter Mh kabwe ameyeandika maneno haya;

Nilipata nafasi kumsalimu @samatta77 jana jioni nyumbani kwake Genk. Nimefurahi kuwa anaendelea vizuri na anapambana kuhakikisha anaendelea kukuza nchi yake na yeye mwenyewe. Ana mawazo mazuri Sana ya kuendeleza soka la Tanzania. Mungu atamsaidia Samata wetu Watanzania
Elimu Yetu

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Edusportstz↑ Grab this Headline Animator

No comments:

Post a Comment