MASAU BWIRE:TUTAIBUKA WASHINDI LEO - EDUSPORTSTZ

Latest

MASAU BWIRE:TUTAIBUKA WASHINDI LEO

Image result for MASAU BWIRE

Afisa Habari wa Klabu ya Ruvu Shooting FC, Masau Bwire, ametamba kuwa kikosi chake kipo
vizuri na kitaibuka na ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar FC huku akitumia neno la 'Tutaipapasa' jioni ya leo katika pambano la Ligi Kuu Bara.

Masau amesema kwa namna mfumo wao na mwenendo walionao hivi sasa, basi Mtibwa itawalazimu wawe na jitihada za dhati kunusuru kipigo leo.

"Mimi nakuambia kwa mfumo tulionao hivi sasa Mtibwa wajiandae na kipigo tu, tutaipapasa tu, wala hawana ugumu wowote, nitafute baada ya dakika 90 kumalizika nikupe matokeo ya ushindi. Tena ulipaswa kuniuliza mtashinda ngapi, wala huna haja ya kuuliza namna mchezo utakavyokuwa" - Bwire.

Mtibwa Sugar nyenye pointi 27 na ikiwa katika nafasi ya 5 ya msimamo wa Ligi, itakuwa mwenyeji wa pambano hilo litakalochezwa kwenye Uwanja wa Manungu mjini Morogoro.

Ruvu Shooting nayo mpaka sasa ina alama 20 huku ikiwa nafasi ya 9 ya msimamo wa Ligi.
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz