Type something and hit enter

On

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga wanaendelea kuwakosa nyota wao muhimu kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Mwadui FC.

Akiongea leo mbele ya wanahabari msemaji wa timu hiyo Dismas Ten amesema wachezaji watakao kosekana katika mchezo huo ni Donald Ngoma, Geofrey Mwashiuya, Thabaan Kamusoko na Obrey Chirwa.

"Tunawachezaji wetu ambao bado ni wagonjwa na wataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Mwadui huku Chirwa atakosekana kwasababu anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu aliyopewa na kamati ya maadili ya TFF'', amesema Ten.

Kwa upande wa mshambuliaji raia wa Burundi Amissi Tambwe, Ten amesema mchezaji huyo amepona Malaria iliyokuwa inamsumbua hivyo kinachosubiriwa ni uamuzi wa Mwalimu kama atampanga kesho.

Yanga inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 21. Mchezo huo wa kesho utachezwa saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. 

BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment