YANGA YA PATA DIRI LA MKATABA WA BILLION 2 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 16 January 2018

YANGA YA PATA DIRI LA MKATABA WA BILLION 2


Mabingwa wateteziwa ligi kuu Tanzania Bara Yanga, leo wamesaini mkataba wa miaka 3 na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo Macron wenye thamani ya bilioni mbili.

Katika mkataba huo uliosainiwa kwenye makao makuu ya klabu hiyo, Yanga itatoa haki zote za utengenezaji na usambazaji wa jezi zao huku pia nembo ya kampuni ya Macron itaanza kuonekana kwenye jezi za Yanga SC.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewaonya wote wanaouza jezi za klabu hiyo bila kuwepo kwa makubaliano na watawachukulia hatua za kisheria kwasababu sasa yupo mwenye haki ya kufanya hivyo. Pia Mkwasa amewakaribisha wawekezaji zaidi ndani ya klabu hiyo.

Naye Mkurugenezi mtendaji wa kampuni hiyo hapa Tanzania Suleiman Karim amewahakikishia wana Yanga kuwa klabu hiyo itapata faida kupitia mauzo ya jezi orijino za klabu.

Kampuni ya Macron inafanya kazi katika nchi zaidi ya 16 duniani zikiwemo England, Italia na Ufaransa. Hivi karibuni kampuni hiyo iliingia mkatata wa miaka 2 na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wenye thamani ya milion 800.EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ