NKAMIA AZIDI KUDAI MUDA WA RAIS KUONGEZA MPAKA KUFIKIA MIAKA 7 - EDUSPORTSTZ

Latest

NKAMIA AZIDI KUDAI MUDA WA RAIS KUONGEZA MPAKA KUFIKIA MIAKA 7



Mbunge wa Chemba kwa tiketi ya CCM, Juma Nkamia amefunguka na kusema amemsikia Rais kuhusu kutohitaji kufanya mabadiliko ya Katiba na kubadili ukomo wa Urais na kudai Rais mwenyewe hawezi kusema anataka kuendelea kuongoza bali watu ndiyo hupelekea hilo.


Juma Nkamia amesema hayo wakati akiongea na kituo kimoja cha habari cha Kimataifa na kudai kuwa ametafakari kauli ya Rais Magufuli na kuomba ushauri kutoka kwa watu na mwisho kusema kuwa yeye haoni tatizo Rais kubadili ukomo wa Rais kutoka miaka 5 mpaka 7 hivyo atazungumza na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai


"Mhe. Rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama changu amesema yeye asingependa na hafurahishwi na hilo jambo sasa mkubwa akishasema wewe uliopo chini unatafakari hoja yako kwanza na unapata ushauri pia lakini mimi nakubaliana na hoja yake. Ila siyo yeye anayetaka kuendelea, mimi kwa mtazamo wangu na kwa kazi anazofanya na nikipita katika maeneo mengi wananchi wanaridhika na utendaji wake na siku zote haiwezekani Rais mwenyewe akasema mimi nataka kuendelea, bali ni wale ambao tunamuangalia utendaji wake wa kazi ndiyo wanaweza kutoa mapendekezo" alisema Nkamia


Mbunge huyo alizidi kusisitiza kuwa "Mimi niseme kwamba sisi wananchi pamoja na mimi na nafasi yangu kama Mbunge na kwa mujibu wa Kanuni na taratibu za Bunge ninaona kwamba Mhe. Rais kubadilisha miaka mitano kwenda saba si jambo la ajabu sana. Hivyo kwa mujibu wa kanuni za Bunge nitazungumza na Mhe. Spika na maelekezo ambayo nitapewa na Spika wa Bunge nitayafanyia kazi" alisema Nkamia


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mnamo tarehe 13 Januari, 2018 alifunguka na kuweka wazi kuwa haridhishwi na hapendi mjadala uliokuwa ukiendelea kuhusu kufanya mabadiliko ya Katiba na kuongeza ukomo wa uongozi kutoka miaka mitano ya sasa na kwenda miaka saba.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE
http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz