MSHAMBULIAJI WAA KENYA AANDIKA HISTORIA MPYA KWENYE LIGI YA HISPANIA - EDUSPORTSTZ

Latest

MSHAMBULIAJI WAA KENYA AANDIKA HISTORIA MPYA KWENYE LIGI YA HISPANIA


Mshambuliaji wa Kenya Michael Olunga aifungia klabu yake ya Girona hat-trick La Liga
Mshambuliaji wa klabu ya Girona nchini Uhispania, Mkenya Michael Olunga ameweka historia siku ya Jumamosi , na kuwa mchezaji wa kwanza wa Kenya kufunga hatrick katika ligi ya Uhispania huku wakiishinda klabu ya Las Palmas 6-0.

Olunga aliingia kama mchezaji wa ziada na kufunga katika dakika ya 57, 70 na 79 na kuwa mshambuliaji wa kwanza wa klabu ya Girona kufunga hat-rick katika msimu wake wa kwanza katika ligi ya La Liga.

Ushindi huo ulikuwa mkubwa kwa klabu hiyo ya Catalan tangu iingie katika ligi ya La Liga.

Olunga mwenye umri wa miaka 23 anaichezea Girona kwa mkopo kutoka klabu ya China ya Guizhou Hengfeng.
Samatta, Olunga na Onyango kuwania taji la mchezaji bora Afrika
Mkenya ajiunga na klabu ya China kwa ksh. 467m
Orodha ya wanaowania taji la mchezaji bora Afrika yatolewa

Girona walikuwa mbele baada ya kipindi cha kwanza kupitia bao la penalti .

Mchezaji huyo wa Kenya alifunga krosi murua iliopigwa na Johan Mojica na kuongeza uongozi wa Girona kabla ya kuchangia katika bao lilofungwa na kiungo wa kati wa klabu hiyo Borja Garcia.

Makosa ya walinzi wa Las Palmas yalimfanya Olunga kuongeza bao la nne kabla ya kumpatia pasi nzuri Cristian Portu aliyefunga bao la 5.

Baadaye Olunga alifunga bao la sita na hat-rick yake ya kwanza kwa urahisi dakika 11 kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz