KISA KILICHOFANYA WENGER KUFUNGIWA HIKI HAPA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 6 January 2018

KISA KILICHOFANYA WENGER KUFUNGIWA HIKI HAPA
Chama Cha soka cha England FA kimetangaza kumfungia kocha wa club ya Arsenal ya England Arsene Wengerkwa kosa la kutoa maneno yasiokuwa ya kiungwana kwa refa Mike Dean baada ya game ya Arsenal dhidi ya West Ham United iliyomalizika kwa sare ya 1-1.Kocha huyo raia wa Ufaransa alikuwa na hasira dhidi ya refa Mike Dean ambaye aliwapa penati ya utata West Ham United katika mchezo uliyochezwa siku ya mwaka mpya, Wenger amefungiwa kosa pia la kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo cha refa Mike Dean.


Wenger akiongea na refa Mike Dean

Wenger ambaye amefungiwa mechi tatu na faini ya pound 40,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 120 baada ya game hiyo alitoa kauli hii ambayo inatafsirika kama kumkosea heshima muamuzi “Maamuzi haya yalikuwa ya kushangaza kidogo, mmemuona (Dean) anafanya anachotaka kitokee, baadhi ya maamuzi msimu huu yamekuwa yakifanywa dhidi yetu sio sawa”

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ