AGIZO LA KALEMANI TANESCO KUGONGA MWAMBA - EDUSPORTSTZ

Latest

AGIZO LA KALEMANI TANESCO KUGONGA MWAMBA



Agizo lililotolewa na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani Desemba 22 mwaka jana kwa mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Tito Mwinuka kutaka jengo la ofisi za makao makuu libomolewe ndani ya siku kumi, halijatekelezeka kama alivyotaka.

Dk Kalemani alitoa agizo hilo Desemba 22 akitaka amri ya Rais John Magufuli ya kubomoa jengo la makao makuu ya Tanesco kupisha upanuzi wa Barabara ya Dar- Morogoro itekelezwe ndani ya siku kumi na kukamilika ifikapo mwisho wa mwezi huo.

Dk Kalemani alitoa agizo hilo Desemba 22 akitaka amri ya Rais John Magufuli ya kubomoa jengo la makao makuu ya Tanesco kupisha upanuzi wa Barabara ya Dar- Morogoro itekelezwe ndani ya siku kumi na kukamilika ifikapo mwisho wa mwezi huo.

Kalemani jengo hilo lililopo Ubungo kushuhudia shughuli ya ubomoaji kutiaa agizo la Rais na akasema hatataka kusikia habari ya sikukuu za Krismasi na mwaka mpya kwa wafanyakazi wa Tanesco.

Kalemani alisema hakuridhishwa na kasi ya ubomoaji na hivyo kulazimika kutoa agizo hilo na kuzuia wafanyakazi wa Tanesco kutosherekea sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya ili kuhakikisha jengo hilo linavunjwa lote kabla ya 31 Desemba mwaka jana.

Hata hivyo, gazeti la Mwananchi jana asubuhi lilitembelea eneo la makao hayo makuu ya Tanesco na kukuta ubomoaji haujakamilika kama ilivyoagizwa na Dk Kalemani.

Mwananchi ilikuta nusu ya jengo hilo, upande wa juu ghorofani ukiendelea kubomolewa.

Jengo hilo limezungushiwa nyavu kwa ajili ya kuzuia madongo yanayoporomoka wakati wa ubomoaji.

Alipotafutwa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco kuzungumzia utekelezaji wa agizo hilo umefikia wapi, alisema hawezi kuzungumzia kitu chochote.

“Nadhani hata wewe una macho. Unaweza ukapita site kuona kinachoendelea. Siwezi kuzungumzia kitu ambacho kipo kwenye utekelezaji” alisema Mwinuka.

Waziri Kalemani hakupatikana.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz