HUYU NDO MTOTO ANAYEITESA KAMPUNI YA H&M - EDUSPORTSTZ

Latest

HUYU NDO MTOTO ANAYEITESA KAMPUNI YA H&M


H&M

Wasanii na wachezaji mashuhuri duniani wamekosoa hatua ya kampuni ya mavazi na mitindo ya H&M kuweka tangazo la mvulana mweusi akiwa amevalia fulana yenye ujumbe ambao umefasiriwa kuwa wa ubaguzi wa rangi.


Fulana hiyo ya rangi ya kijani ilikuwa na ujumbe "coolest monkey in the jungle", kwa maana ya tumbili mtanashati au bora zaidi porini.

Mwanamuziki Diddy na mchezaji wa Manchester United Romelu Lukaku wamechukua hatua ya kupakia picha zenye ujumbe mbadala.

Mwanamuziki Abel Makkonen Tesfaye, maarufu kama The Weeknd, amesema hatafanya kazi tena na kampuni ya mavazi na mitindo ya H&M baada ya tangazo hilo.

The Weeknd amesema tangazo hilo limemuacha na "mshangao na aibu kubwa".

Mwanamuziki huyo awali amewahi kuuza bidhaa zenye nembo yake kupitia H&M na pia kuwatangazia bidhaa zao.

Ameandika kwenye Twitter kwamba amekerwa sana na picha hiyo.

H&M wamesema: "Tunasikitika sana kwamba picha hiyo ilipigwa, na tunajutia sana kwamba ilisambazwa.


Haipatikani tena

"Kwa hivyo, tumeagiza iondolewe kutoka kwenye majukwaa yetu yote, na kwamba fulana hizo zisiuzwe tena."Haki miliki ya pichaH&M WEBSITE

Rapa na produsa Diddy aliongeza ujumbe wa "coolest king in the world" (mfalme bora zaidi duniani).

Diddy aliandika kwenye Twitter: "Weka heshima kiasi".


Haipatikani tena

Lukaku aliweka ujumbe wa "black is beautiful" (weusi ni maridadi) na kuandika "Wewe ni mwanamfalme na utakuwa mfalme karibuni."

Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa rlukaku9

Mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James aliweka ujumbe "King of the world" (Mfalme wa Dunia) na kumvika mvulana huyo taji.

Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa kingjames

Aliandika: "Sisi Wamarekani Weusi lazima kila wakati tutahitajika kuruka vizuizi, kuwathibitishia watu kwamba wamekosea na kutia bidii hata zaidi kuthibitisha kwamba tunastahiki".

Wengine wamekuwa wakizungumzia picha hiyo mtandaoni.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.

 BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz