UGANDA YAFUTA KIKOMA CHA UONGOZI WA RAIS - EDUSPORTSTZ

Latest

UGANDA YAFUTA KIKOMA CHA UONGOZI WA RAIS


Rais Yoweri Museveni sasa anaweza kuwania urais tena mwaka 2021

Wabunge wa Uganda wameyapitisha mabadiliko ya Katiba ambayo sasa yanamruhusu Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa kwa muhula wa sita.

Baada ya siku tatu za majadiliano mazito na mivutano, hatimaye waondoa ukomo wa umri wa miaka 75 kwa mgombea urais. Wabunge wa upinzani walitoka ndani ya ukumbi zaidi ya mara moja na sita kati yao walifukuzwa ukumbini kutokana na kuupinga muswada. Na hatimaye spika wa bunge hilo Bi Rebecca Kadaga akitangaza matokeo baada ya kupiga kura ya mwisho ikiwa wapiga kura wawili hawakuwa na upande, upinzani wamepata kura 62 na wanaotaka kuondowa kikomo kura 315 na hivyo Spika kutangaza kuwa mswaada huo umepita baada ya kusomwa mara ya tatu.Haki miliki ya pichaBUNGE LA UGANDAImage captionWabunge wa Uganda

Wabunge pia wamerejesha ukomo wa vipindi viwili vya kukaa madarakani kutoka miaka saba hadi miaka mitano, kwa hivyo wabunge wa sasa wataendelea kuongoza hadi mwaka 2023.

Ni pengine kutokanana malalamiko kuwa kuondolewa kwa ukomo wa umri kunaweza kumfanya Bwana Museveni kuwa Rais wa milele. Wafuasi wa Museveni wanadai ni waganda ndiyo wanaweza kumwondoa madarakani kwa Kura.

Upande wa upinzani waliweka pingamizi kuzuia mswaada huo usipite lakini idadi yao katika bunge ni ndogo, kiongozi wa wabunge wa upinzani Winne Kiiza amesikitishwa na kupitishwa mswaada huo.

Lakini upande wa chama tawala ulitumia kila mbinu kuona kwamba mswaada huo unapita ili Rais Museveni kuendelea kutawala .

Kupitishwa mswaada huo kunampatia tena Rais Museveni kutawala miaka mingine 14 kulingana na mswaada huo, lakini raia wa Uganda wengi walikuwa hawaungi mkono kubadilishwa kwa katiba kumuongeza Rais Museveni kutawala baada ya kutawala zaidi ya miongo mitatu.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz