NETANYAU AFUNGUKA JUU YA MJI MKUU JERUSALEM - EDUSPORTSTZ

Latest

NETANYAU AFUNGUKA JUU YA MJI MKUU JERUSALEM


 Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3000 asema netanyau

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa wapalestina ni lazima wakubali kuwa Jurusalem ndio mji mkuu wa Israel ili amani iweze kupatikana.

Netanyahu alisema Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3,000 na haujakuwa mji mku wa watu wengine.

Aliongea huku maandamano yakiendelea kwenye ulimwengu wa kiislamu kufuatia hatua ya Marekani kuutambua Jurusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Ghasia zilizuka karibu na ubalozi wa Marekani nchini Lebanon na kwingineno siku ya Jumapili.


Jerusalem kwenyewe, mpalestina mmoja alikamatwa kwa kumdunga kisu na kumjeruhiwa vibaya afisa wa usalama wa Israel karibu na kituo kimoja cha basi.

Akiongea mjini Paris baada ya mazungumzo na rais wa Ufaransa Emmauel Macron, Bw Netanyahu alisema kuwa jitihada za kuwanyima wayahudi mji wa wa Jerusalem ni kitu kibaya.

"Unaweza kusoma katika kitabu kizuri zaidi, kinaitwa Biblia, alisema. Unaweza kuyaskia katika historia ya jamii wa wayahudi kote duniani… Ni wapi tena kuna mji wa Israel, isipokuwa Jerusalem?

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz