-->

Type something and hit enter

OnWema Sepetu na Makonda.

BAADA ya madai ya muda mrefu juu ya uwepo wa bifu kati ya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, hatimaye wikiendi iliyopita wawili hao walikutana uso kwa uso ‘live’.

Vyanzo mbalimbali vililieleza Ijumaa Wikienda kuwa, baada ya Wema kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekuwa karibu mno na viongozi wa chama hicho akiwemo mkuu huyo wa mkoa.

“Wema na Makonda sasa hivi mambo ni supa siyo dizeli. Yale yote yaliyotokea kipindi cha nyuma ilikuwa ni kama ajali kazini maana sasa hivi wapo tayari kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo na kujenga nchi,” kilisema chanzo chetu.


Alicokiandika Wema kwenye Instagram yake.

Jana, Ijumaa Wikienda lilishuhudia mrembo huyo akitupia picha mfululizo katika akaunti yake ya Instagram zilizomwonesha akiwa na Makonda huku picha hizo zikisindikizwa na maneno haya: “Nipo na kaka yangu, kamanda mwenyewe, anaitwa Mr Dar es Salaam, tunakutakieni Jumapili njema…”

Baada ya kujinea mambo mubashara, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Wema na Makonda kupitia simu zao za mkononi ili kuzungumzia hatua hiyo ambapo simu ya Wema iliita bila kupokelewa, huku ile ya Makonda ikiwa haipatikani.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Makonda aliwataja watu mbalimbali wanaodhaniwa kuhusika na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya ambapo katika listi hiyo jina la Wema lilikuwepo, jambo lililomtibua mlimbwende huyo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment