Type something and hit enter

On


Ole Sosopi akimjulia hali Lissu.
MBUNGE wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ambaye sasa Kenya akiendelea na matibabu kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017 amefunguka juu ya viongozi ambao wanakisaliti CHADEMA na kusema jambo hilo lisiwatishe bali wao waendelee na kazi yao.

Tundu Lissu aliyasema hayo jana alipoonana Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Taifa, Patrick Ole Sosopi ambaye alimtembelea Mhe Lissu hospitali jijini Nairobi jana kumjulia hali

“Ndugu zangu Mhe Lissu ameweza kunieleza mambo mengi sana na binafsi naamini ameniagiza kwa niaba ya Baraza la Vijana na tutayetekeleza kwa maslahi mapana ya nchi na chama chetu, hajasita kuniambia kwamba hali ya siasa yetu ndani ya nchi yetu kwa biashara inayoendelea kununua Viongozi uchwara na wenye tamaa wa chama chetu, amesema tusipate hofu CHADEMA hatujaanza kusalitiwa leo na hao wanaondoka, sio ajabu hata kidogo kwani mbona Yesu aliwahi kusalitiwa tena na mwanafunzi wake na hakuacha kazi yake” aliandika Ole Sosopi.


Aidha Sosopi aliendelea kusema kuwa Tundu Lissu amemweleza kuwa hata watu ambao waliwahi kuisaliti CHADEMA kipindi cha nyuma hawajapata mafanikio yoyote katika maisha yao


“Wanaotusaliti hawajawahi kuwa na mafanikio katika maisha yao, tusikate tamaa mapambano yaendelee. Mwisho kabisa Mhe. Lissu ametuma salamu nyingi kwa Watanzania wote wanaoendelea Kumchangia na Kumuombea, ameendelea kuwasihi waendelee kumchangia na kumuombea, maana Bunge na serikali wamekataa kabisa kumtibia ili hali kwa mujibu wa sheria ni haki yake,” alisema Ole Sosopi.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment