LISSU AFUNGUKA JUU YA SHAMBULIZI lAKE - EDUSPORTSTZ

Latest

LISSU AFUNGUKA JUU YA SHAMBULIZI lAKE


Mwanasheria kuu wa chama upinzani Chadema nchini Tanzania Tundu Lissu, ambaye amekuwa akipokea matibabu Nairobi tangu alipopigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwezi Septemba, amesema anaamini kushambuliwa kwake kulihusiana na siasa nchini humo.


Akizungumza na BBC, mbunge huyo wa Singida Mashariki amelilaumu Bunge la nchi hiyo akisema halijachukua hatua zozote kumsaidia tangu kulazwa kwake hospitalini.

Makamu wa Rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu alimtembelea hospitalini mapema wiki hii.

Bw Lissu amesema anaendelea kupata nafuu vyema.

Juhudi za BBC za kuwasiliana na msemaji wa Bunge la Tanzania kuhusu tuhuma za Bw Lissu hazijafua dafu.

Amezungumza na mwandishi wa BBC John Nene.EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz