LISSU AANZA KUTENGAMAA; ASIMAMA KWA MARA YA KWANZA TANGU KUSHAMBULIWA KWAKE - EDUSPORTSTZ

Latest

LISSU AANZA KUTENGAMAA; ASIMAMA KWA MARA YA KWANZA TANGU KUSHAMBULIWA KWAKE


Tundu Lissu asimama kwa mara ya kwanza akiwa hospitalini Nairobi

Mwanasheria mkuu wa chama upinzani Chadema nchini Tanzania Tundu Lissu, ameweza kusimama kwa mara ya kwanza baada ya kushambuliwa.

Tundu Lissu amekuwa akipokea matibabu Nairobi tangu alipopigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwezi Septemba.

Katika picha iliowekwa katika ukurasa wa Facebook wa CHADEMA, mbunge huyo anaonekena akisimama akisaidiwa na wahudumu wawili wa hospitali.

Ujumbe ulioambatana na picha ukisema "Wiki iliyopita niliwataarifu kwamba madaktari wangu wamesema 'nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania.Leo Boxing Day (Tarehe 26 Disemba) nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa 'Mababa Cheza' wangu. Hatua inayofuata ni magongo kesho na nitawajulisheni hatua nyingine katika matibabu yangu."

Bwana Lissu ambaye pia ni mkuu wa chama cha mawakili nchini Tanzania amekuwa akizozana na serikali ya Rais Magufuli na alikamatwa mara sita mwaka huu pekee, akishtumiwa kwa kumtusi kiongozi huyo wa taifa mbali kuharibu usalama wa umma, miongoni mwa mashtaka mengine.amesema anaamini kushambuliwa kwake kulihusiana na siasa nchini humo.

Akizungumza na BBC hivi karibuni mbunge huyo wa Singida Mashariki amelilaumu Bunge la nchi hiyo akisema halijachukua hatua zozote kumsaidia tangu kulazwa kwake hospitalini.

Makamu wa Rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu alimtembelea hospitalini mwezi Novemba.
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz