ZANU PF YAMVUA UONGOZI MUGABE - EDUSPORTSTZ

Latest

ZANU PF YAMVUA UONGOZI MUGABE


ZANU PF inaelezwa kwamba imeanza mchakato wa kumwondolea urais Mugabe.

Chama cha ZANU PF cha Zimbabwe kimemvua uongozi wa chama hicho, Rais Robert Mugabe na kumchagua aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Mnangagwa kukiongoza.

Rais Mugabe alimuondoa madarakani Mnangawa wiki mbili zilizopita hivyo kuibua matukio kadhaa, likiwemo la jeshi kutwaa madaraka na kumzuia Mugabe (93), kumteua mkewe Grace kuwa makamu wa rais.

Wazimbabwe jana Jumamosi Novemba 18,2017 walishiriki maandamano kupinga utawala wa Rais Mugabe ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Rais Mugabe anatarajiwa kukutana na viongozi wa jeshi la nchi hiyo na tayari msafara wa magari umeonekana ukitoka nyumbani kwake.

Kiongozi wa chama cha maveterani wa vita ya ukombozi wa Taifa hilo, Chris Mutsvangwa ameliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba, chama hicho pia kimeanza mchakato wa kumwondoa Mugabe kama Rais wa nchi hiyo.

Reuters imeripoti kwamba Grace, mkewe Mugabe amefukuzwa uanachama.

Watu wameonekana mitaani wakicheza na kushangilia baada ya ZANU PF kumwondoa katika uongozi Mugabe. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz