SIRI YA MOURINHO KUMBANIA RONALDO YAFICHUKA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 19 November 2017

SIRI YA MOURINHO KUMBANIA RONALDO YAFICHUKA

 ronaldoMADRID, HISPANIA. Kumbe kutua au kutotua kwa Cristiano Ronaldo pale Manchester United kunategemea kama Jose Mourinho atakuwa tayari kujumuika na mchezaji huyo kwa mara nyingine. 

Taarifa kutoka Hispania zinasema kwambaM mchezaji huyo alipokataa kusaini mkataba mpya aliweka wazi kuwa anataka kuuzwa kwenda England. 

Imefahamika kuwa viongozi wa Manchester United wamemwambia Mourinho amuweke mchezaji huyo kwenye mipango ya kumrudisha baada ya kushindwa kutamba katika Ligi Kuu kwa misimu kadhaa tangu kuondoka kwa kocha Alex Ferguson.

  Tangu kuondoka kwa Ferguson kikosi hicho kimemaliza katika nafasi ya saba, ya nne, ya tano na ya sita kwenye Ligi Kuu.

  Ukiachana na Ronaldo klabu hiyo pia inawafuatilia kwa karibu nyota wa Valencia, Carlos Soler, winga Emil Forsberg, Antoine Griezmann na Gareth Bale Hata hivyo inaaminika kwamba Mourinho anasita kutoa nafasi ya Ronaldo kwa sababu nyota huyo ana umri wa miaka 32. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment