UGIRIKI YA YACHAPWA NA CROTIA MCHEZO WA MTOANO KUELEKEA KOMBE LA DUNIA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 10 November 2017

UGIRIKI YA YACHAPWA NA CROTIA MCHEZO WA MTOANO KUELEKEA KOMBE LA DUNIA

Nahodha wa Croatia Luka Modric

Timu ya taifa ya Croatia imepata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ugiriki katika mchezo wa mtoano wa mkondo wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia.

Magoli ya Croatia yalifungwa na Luka Modric aliyefunga kwa mkwaju wa penati, Nikola Kalinic akaongeza goli la pili, mshambuliaji Ivan Perisic akaongeza goli la tatu.

Mshambuliaji Andrej Kramaric akahitimisha kazi kwa goli na nne goli pekee la Urigiki katika mchezo huo lilifungwa na Sokratis Papastathopoulos

Switzerland wakicheza ugenini wamewafunga Ireland Kaskazini kwa bao 1-0 bao lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Ricardo Rodriguez.

Michezo ya Marudiano kwa timu hizi itachezwa Novemba 12 na washindi wa jumla watafuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno