MATOKEO MICHEZO YA KIMATAIFA YA KIRAFIKI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 10 November 2017

MATOKEO MICHEZO YA KIMATAIFA YA KIRAFIKI
Wachezaji wa Uholanzi wakishangia goli

Michezo ya kimataifa ya kirafiki imechezwa usiku wa kuamkia leo katika viwanja tofuti Uholanzi wameibuka na ushindi wa bao 1 -0 dhidi ya Scotland, mshambuliaji Memphis Depay akifunga goli hilo.

Romania wakataka mbele ya Uturuki kwa kuwafunga kwa mabao 2-0 magoli yote mawili ya Romania yalifungwa na kiungo Gheorghe Grozav.

Luxembourg wakicheza nyumbani wameibuka kidedea kwa kuwafunga Hungary kwa magoli 2-1, Aurelien Joachim ndie aliyeanza kuwapatika Luxembourg goli kwa kuongoza katika dakika ya 15 ya mchezo.

Katika dakika ya 18 Hungary wakasawazisha goli hilo kupitia kwa Nemanja Nikolic, zikiwa zimesalia dakika tisa mchezo kumlizika Marvin Santos akaongeza bao la pili kwa upande wa Luxembourg

Matokeo mengine ya michezo hiyo ya kimataifa ya kirafiki ni

Cambodia 1 - 2 Myanmar

Singapore 0 - 1 Lebanon

Hong Kong 0 - 2 Bahrain

Armenia 4 - 1 Belarus

Finland 3 - 0 Estonia

FTPanama 1 - 2 Iran

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment