TAZAMA KILICHOJILI MBAKA SASA KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2018 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 9 November 2017

TAZAMA KILICHOJILI MBAKA SASA KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2018
Katika bara la Ulaya zimebaki timu 4 tu ambazo zitacheza michezo yao wiki hii ili kupata timu itakayoenda kombe la dunia, bara la Afrika bado tatu na mbili kutoka bara la Amerika na Asia, na hii ndio michezo itakayoamua timu hizo 9.

Crotia vs Ugiriki. Sio mchezo rahisi kwa Luka Modric na wenzake kwani Ugiriki wameshafudhu kwenye michuano hii mara 5 na wana uzoefu, Alhamisi utapigwa mchezo wa kwanza kabla ya kurudiana siku ya Jumapili.

N.Ireland vs Switzerland. Northern Ireland kama wakafanikiwa kuwafunga Switzerland katika mchezo huu, watakuwa wamefudhu kwa mara ya kwanza katika michuano hii tangu wafanye hivyo mwaka 1986.

Sweden vs Italy. Itakuwa aibu kwa taifa bingwa mara 4 wa michuano hii timu ya taifa Italia kama watashindwa katika hatua hii ya mtoano, Alhamisi Italia watasafiri hadi Sweden kabla ya kurudi Millan siku ya Jumapili kuamua hatma yao.

Dermanrk vs Ireland. Mechi ya kutafuta heshima kwa pande zote mbili lakini tofauti na wengine nu kwamba hawa wataanza mchezo wao wa kwanza siku ya Jumamosi November 11 kabla ya kurudiana siku ya Jumanne November 13.

New Zealand Vs Peru. Toka mwaka 1982 timu ya taifa ya Peru hawajawahi kwenda kombe la dunia na Jumamosi hii wanakwenda kukabiliana na New Zealand huku nahodha wao Paolo Guerrero akiwa hayupo.

Hondurus vs Australia, Australia watakuwa na kibarua kigumu kwani timu ya taifa ya Hondurus wana rekodi nzuri katika kwenda kombe la dunia ambapo mara mbili mfululizo wamefudhu, na Jumamosi Hondurus wakiwa nyumbani watajaribu kufudhu kwa mara ya tatu.

AFRICA, Katika bara la Africa tayari timu mbili Nigeria na Misri wameshatangulia katika michuano hiyo itakayopigwa mwakani nchini Urusi na sasa kumebaki timu tatu ili kukamilisha idadi ya timu tano.

Group A. Tunisia wanaongoza kundi kwa tofauti ya alama 3 na wanahitaji suluhu vs Libya kwenda Urusi lakini wakipoteza mechi yao huku DR Congo wakimfunga Guinea baasi mshindi ataamuliwa kwa tofauti ya mabao.

Group B. Morocco wanaongoza kundi wakifuatiwa na Ivory Coast, lakini Morocco wanakwenda Abidjan kuwakabili Ivory Coast huku Ivory Coast wakihitaji alama zote tatu ili kwenda katika michuano ya kombe la dunia.

Group D. Kimbembe kimo hapa kwani timu zote nne zinaweza kufudhu kombe la dunia, Novemeber 10 Senegal wataikaribisha Bafanabafana na Senegal anahitaji ushindi ili kwenda kombe la dunia.
Lakini endapo Senegal na Bafanabafana watasuluhi mechi moja na Senegal akapoteza nyingine baasi mshindi katika mechi kati ya Cape Verde na Burkina Faso anaweza kwenda hadi nafaso ya kwanza kwa tofauti ya mabao huku Burkina Faso wakiwa katika nafasi nzuri kweny hili.


Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno