-->

Type something and hit enter

OnBaada ya timu ya taifa ya Misri na Nigeria kutangulia kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia 2018, hii leo timu ya taifa ya Senegal nayo imekata tiketi kuelekea michuano hiyo.

Senegal wamekata tiketi hiyo baada ya kushinda mabao mawili kwa nunge dhidi ya timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana katika mchezo uliopigwa mjini Polokwane nchini Afrika Kusini jioni ya leo.

Alikuwa ni Diafra Sakho alieyanza kuwafungulia Senegal ukurasa wa mabao dakika ya 12 kabla ya Thamsanq Mkhize kujifunga dakika ya 36 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa wageni kupata ushindi wa mabao mawili.

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Sadio Mane alikuwa chachu ya ushindi wa leo wa Senegal kwani achilia mbali assist ya bao la kwanza pia alikuwa chanzo cha Afrika Kusini kujifunga katika mchezo huo.

Kocha wa timu ya taifa ya Senegal Aliou Cisse anaingia katika vitabu vya rekodi Senegal kwani mwaka 2002 aliipeleka Senegal kombe la dunia yaliyofanyika Korea/Japan kama mchezaji na mwaka huu anaipeleka tena akiwa kama kocha.

Sasa Afrika tayari kumeshapatikana wawakilishi watatu (Nigeria, Misri na Senegal) na sasa kunasubiriwa timu mbili ili kukamilisha idadi kamili ya wawakilishi 5 watakaotuwakilisha katika fainali za kombe la dunia.Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

Click to comment
 
Blog Meets Brand