SINGIDA UNITED YATAMBA KIFUA MBELE - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 17 November 2017

SINGIDA UNITED YATAMBA KIFUA MBELE

 Singida Utd yaona mwezi Namfua

Baada ya ukame wa ushindi katika michezo mitano hatimaye Singida United imerejesha furaha kwa mashabiki wake baada ya kuichapa Lipuli bao 1-0.


Katika mchezo huo uliofanyika leo, Ijumaa kwenye Uwanja wa Namfua Singida, bao pekee la wenyeji

Singida United lilifungwa na Danny Usengimana dakika ya 82.

Kuingia kwa bao hilo kuliamsha kelele kutoka kwa mashabiki wengi waliofurika uwanjani kuipa

sapoti Singida United huku kocha wa kikosi hicho Hans Pluijm akionekana mwenye furaha zaidi.

Nahodha wa Singida United, Mudathir Yahaya alisema wanashukuru kupata ushindi huo na

wanaamini wamewapa furaha mashabiki wao.

"Tunashukuru kupata ushindi kwenye uwanja wa nyumbani.tulipata wakati mgumu kipindi cha

kwanza kwa sababu tulifata mpira wa taratibu waliokuwa wakicheza wapinzani wetu lakini

tulivyoingia vyumbani kocha alituambia tunatakiwa kubadilika na kuwapiga presha wa soka la

haraka ili kuweza kupata bao, "alisema Mudathir.

Naye mshambuliaji wa Lipuli, Seif Karihe alisema hawakuwa na mchezo mzuri kwani walshindwa

kutengeneza nafasi nyingi katika mchezo huo tofauti na wanavyofanya katika michezo mingine

iliyopita.
Singida united iliifululiza kupata sare katika michezo mitano iliyopita na mara ya mwisho kupata

ushindi ilikuwa Septemba 24 ilipoichapa Kagera Sugar bao 1-0.
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment