ARSENAL NA TOTETENHAM JINO KWA JINO BILA CHENGA: WENGER ATIA MKWARA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 17 November 2017

ARSENAL NA TOTETENHAM JINO KWA JINO BILA CHENGA: WENGER ATIA MKWARA

 ARSENAL VS TOTTENHAM
London itasimama hakuna ubishi wakati Arsenal itakapowakaribisha majirani zao Tottenham Hotspur kwenye Uwanja wa Emirates kesho.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema wala huhitaji kuwapa vitisho mastaa wako kwamba, utawanyonga ndiyo watake kushinda mechi hiyo. Yani hii ni wao wenyewe 'automatically' watataka kushinda kipute hicho cha London derby.

Wenger alisema hivyo akijibu swali kwamba, mastaa wake wa sasa waliopo kwenye kikosi hicho huwa hawana moyo wa kupambana kwa ajili ya kuisaidia timu kushinda mechi zake.

 Gwiji la Arsenal, Lee Dixon alitoa ushuhuda wa ugumu wa mechi hiyo akidai wakati anakwenda Arsenal mechi yake ya kwanza dhidi ya Spurs, basi wachezaji wenzake walimkunja shati na kumkandamiza ukutani kwenye vyumba vya kubadilishia wakimwambia asithubutu kufanya makosa kwenye mechi dhidi ya Spurs, ole wake timu ikishindwa. 

Wenger ameisimamia Arsenal kwenye mechi 50 za London derby — ameshinda 22, sare 20 na amepoteza nane tu na anaamini wachezaji wake watapambana kiasi cha kutosha kuwashinda mahasimu wao hao ambao, wanapewa nafasi kubwa ya kushinda msimu huu.

 Wachambuzi wa masuala ya michezo wanadai kwamba, kama ingekuwa kupanga kikosi kinachotokana na mastaa waliopo kwenye timu hizo kwa sasa na ubora wao wa uwanjani, basi Arsenal ingekuwa na wachezaji wasiozidi wawili. Wakati mashabiki wa Ligi Kuu England wakisubiri mechi hiyo ya kukata na shoka, ligi hiyo iliyokuwa mapumzikoni kupisha mechi za kimataifa, itashuhudia pia mechi nyingine kali wakati Bournemouth watakapowakaribisha Huddersfield, Leicester City watawaalika vinara Manchester City huku Chelsea wakiwa ugenini kwa West Brom. 

Liverpool wao watakuwa na shughuli pevu dhidi ya Southampton na Burnley watacheza na Swansea City, Crystal Palace na Everton, wakati vijana wa Jose Mourinho, Manchester United watakuwa nyumbani Old Trafford kuikaribisha Newcastle United ya Rafa Benitez. Mechi hii itakutanisha wapinzani wawili, Benitez na Jose Mourinho. Keshokutwa Jumapili, Watford watacheza na West Ham na Jumatatu, Brighton watakuwa nyumbani kuwakaribisha Stoke City.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno