MKUU WA SOKA ZA ZAMANI ASHITAKIWA KWA RUSHWA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Friday, 17 November 2017

MKUU WA SOKA ZA ZAMANI ASHITAKIWA KWA RUSHWANicolás Leoz ameliongoza shirikisho la soka Amerika ya Kusini kwa miaka 27

Jaji mmoja nchini Paraguay ameruhusu upelelezi kuanza kwa mkuu wa zamani wa shirikisho la soka la Amerika ya Kusini Nicolas Leoz kwa tuhuma za rushwa.

Leoz ni mmoja ya watuhumiwa wakubwa wa rushwa waliotajwa na mahakama moja nchini Marekani.

Bosi huyo wa zamani wa FIFA amekuwa chini ya uangalizi mkali nyumbani kwake Asuncion Paraguay.

Anatuhumiwa pia kupokea rushwa ili kuiruhusu Qatar kuandaa kombe la dunia mwaka 2022.

Leoz anasema tuhuma hizo ni za uongo huku mwanasheria wake akiapa kukata rufaa.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno