SERIKALI YADAI MBOWE ANAPOTOSHA UMMA, SOMA HAPA UJIONE - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 14 November 2017

SERIKALI YADAI MBOWE ANAPOTOSHA UMMA, SOMA HAPA UJIONE

Freeman Mbowe

Waziri Mhagama ameeleza bungeni kuwa Mbowe anatoa kauli za kupotosha kuhusu uteuzi wa Rais.


Waziri Mhagama ameeleza bungeni kuwa Mbowe anatoa kauli za kupotosha kuhusu uteuzi wa Rais

Dodoma. Serikali imemjia juu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kutokana na kauli yake kuwa Rais John Magufuli amekuwa akipendelea baadhi ya kanda katika uteuzi wake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenister Mhagama leo Jumatatu jioni amesema Mbowe anapotosha na kumtaka aache kuingilia madaraka ya Rais.

Wakati akichangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2018/2019, Ijumaa iliyopita Mbowe alienda mbali na kudai anaweza kuleta uthibitisho kama Bunge litamkata kufanya hivyo.

“Mumwambie bwana mkubwa unapoamua mambo mengine tenda haki pande zote. Lakini unapokuwa haki hiyo unaipeleka mahali fulani na unakandamiza upande mmoja unawanyima haki”

Mbowe alitolea mfano wa teuzi mbalimbali alizozifanya Rais Magufuli tangu aingie madarakani mwaka 2015, akisema hazikugawanywa kwa usawa wa mikoa kama utamaduni uliokuwepo awamu zilizopita.

Hata hivyo, leo Jumatatu jioni Jenister amesema Ibara ya 36 (1) (2)(3)(4) imempa Rais madaraka ya kuanzisha na kufuta ya nafasi za mbalimbali kwa utumishi na haijasema atazingatiwa usawa wa kanda.

“Ibara hiyo haisemi kuwa Rais wakati atakapokuwa anafanya uteuzi eti aangalie ukanda. Haisemi hivyo Ibara hiyo haisemi anavyoandaa uteuzi aaangalie makabila mbalimbali,”amesema Mhagama.

“Unasimamaje ndani ya Bunge kuhoji madaraka ambayo Rais amepewa kwa mujibu wa Katiba? Alihoji Mhagama na kutoa mifano ya teuzi tatu zilizofanywa na Rais kutoka mikoa ya Kaskazini.

“Ameteuliwa Aggrey Mwandry kutoka Siha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na anafanya kazi vizuri sana. Ameteuliwa Alexander Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara,”amesema na kuongeza

“Ameteuliwa Anna Kilango kutoka Same. Nina orodha ndefu lakini uteuzi huo unafuata madaraka ya kikatiba. Niwaombe sana wabunge tusiingile madaraka ya Rais aliyopewa kwa mujibu wa Katiba.”Amesema Rais amekuwa akifanya teuzi mbalimbali kwa utashi wa hali ya juu na anateua watu wa kubeba dhamana ya kumsaidia kuongoza kwa niaba yake pasipo upendeleo. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment