HANS POPPE:SISI HATUWEZI KUENDELEA KUMLIPA MTU AMBAYE HACHEZI - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 13 November 2017

HANS POPPE:SISI HATUWEZI KUENDELEA KUMLIPA MTU AMBAYE HACHEZI


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema beki wao Shomari Kapombe anatakiwa kuanza kucheza la sivyo anaweza kwenda.


Hans Poppe amesema Simba haiwezi kuendelea kumlipa mchezaji ambaye hawatumikii.


“Vipimo vinaonyesha Kapombe amepona, vizuri akaanza kucheza. Hata sisi hatuwezi kuendelea kumlipa mtu ambaye hachezi.


“Sasa tunamuachia yeye, arejee acheze au kama vipi basi aende akajiuguze hadi atakapopona,” alisema Hans Poppe.


Kapombe ameendelea kuwa nje ya uwanja tokea amejiunga na Simba akitokea Azam FC.

Beki huyo wa zamani wa Simba amekuwa akiendelea kujitibia kutokana na majeraha yake.
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment