BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 14 November 2017

SARE YA ITALIA NA SWEEDENI YAWATUPA NJE ITALIA


Mara ya mwisho Italia kushindwa kufuzu kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 1958

Mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italia, wameshindwa kufuzu fainali za mwa 2018 nchini Urusi ikiwa ni mara ya kwanza tokea mwaka 1958 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Sweden.

Hii ina maana kwamba Azzurri watayakosa mashindano hayo kwa mara ya pili tokea kuanzishwa, mara ya kwanza ilikua mwaka 1930.Image captionbaada ya mchezo huo mlinza mlango wa muda mrefu Gianluigi Buffon ametangaza kustaafu soka la kimataifa

Kiungo Jakob Johansson wa Sweden aliyefunga goli katika mzunguko wa kwanza alikuwa katika kiwango bora na kuwadhibiti vyema Italia katika uwanja wa San Siro.

Wengi walitaraji Italia kushinda mchezo huu kwa sababu lukuki ikiwemo historia sambamba na kucheza nyumbani.

Italia walitawala mchezo kwa asilimia 75 na kupiga mashuti 27 lakini bahati haikuwa upande wao.Image captionMara ya mwisho Sweden kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 2006

Nusura mshambuliaji Stephan El Shaarawy aandike bao lakini juhudi za mlinda mlango wa Sweden Robin Olsen zilizima ndoto yake.

Matokeo haya yanaifanya Sweden kushiriki mashindano haya tokea mwaka 2006 waliposhiriki kwa mara ya mwisho.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment