AT ATWAA TUZO MBILI MAREKANI - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 14 November 2017

AT ATWAA TUZO MBILI MAREKANI


AT Atwaa Tuzo Mbili Marekani

Msanii wa muziki wa mduara Bongo, AT amefanikiwa kushinda tuzo mbili za B&K Music & Video Music Awards za nchini Marekani ambazo zinahusisha muziki na filamu.

Katika tuzo hizo ambazo zilifanyikakatika mji wa Washington DC, AT ameshinda tuzo hizo kupitia wimbo wake ‘Sili Feel’ ambapo alikuwa akiwania katika vipengele viwili huku kimoja kikiwa ni International Artist ambapo alikwa akiwania na wasanii wengine watatu.

Kipengele kingine ambacho alikuwa anawania msanii huyo ni Best Music Video ambapo alikuwa anawania tuzo hiyo na wasanii wengine 9.

Akiongea na Bongo5, msanii huyo amesema kwa sasa bado yupo nchini Marekani anamalizia kazi zake nyingine za muziki akiwa na uongozi wake mpya uitwao Dashiam Management ambao ndio unasimamia kazi zake kwa sasa.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment