TETESI ZA SOKA LA ULAYA TAR 14.11.2017 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Tuesday, 14 November 2017

TETESI ZA SOKA LA ULAYA TAR 14.11.2017GETTY IMAGESImage captionGareth Bale

Real Madrid wameamua kumuuza mshambuliaji wa Wales, Gareth Bale, 28, mwishoni mwa msimu. (AS - in Spanish)

Aliyekuwa mchezaji wa Tottenham na Southampton Bale anaweza kurejea katika Premier League ikiwa atafurahia kufanya hivyo. (Mirror)AFPImage captionNabil Fekir

Arsenal wanakaribia kukamilsha dili ya kumsajili mshambuliaji wa Lyon, Nabil Fekir kwa pauni milioni 60 ambaye kuwasili kwake kutafufua kuondoka kwa Mesut Ozil, 29 na Alexis Sanchez, 28.

Mshambualiaji wa Atletico Antoine Griezmann amesema kuwa ana nia ya kuhamia Paris St-Germain. Anasema kuwa kucheza klabu moja na Neymar na pia Kylian Mbappe itakuwa ndoto. (Telefoot via the Independent)Emre Can

Borussia Dortmund wana naia ya kumsaini mchezaji wa Liverpool Emre Can, huku mkataba wa mchezaji huyo wa kiungo cha kati mwenye miaka 23 ukitarajiwa kukamilika mwishoni wa msimu. (Times - subscription required)

Rangers wanamwinda meneja wa Northern Ireland Michael O'Neill, 48, ambaye pia anatafuwa na Scotland. (Telegraph)

Meneja wa Wales Chris Coleman, 47, ataihama timu ya taifa ikiwa chama cha kandanda cha wales, hakitawapa mikataba ya kudumu wafanyakazi wenzake (Star)Ahmed Musa

Mshambuliaji wa Leicester City Mnigeria Ahmed Musa, 25, huende akahamia Hull City mwezi Januari. (sport-express.ru)

Mshambuliaji wa Bolton Wanderers Gary Madine, 27, anataka mshambuliaji mwenzake Adam Armstrong, 20, kubaki klabu hiyo kwa mkopo kutoka Newcastle United. (Bolton News)

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno