RAIS MPYA WA ZIMBABWE EMERSON D. MNANGAGWA KUAPISHWA LEO - EDUSPORTSTZ

Latest

RAIS MPYA WA ZIMBABWE EMERSON D. MNANGAGWA KUAPISHWA LEO



Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu.


…Akipigiwa wimbo wa taifa baada ya kuapishwa.


Askari wakipiga mizinga ya heshima katika uapisho huo.


Rais Mnangagwa na mkewe Auxillia wakiwa wakiwasalimia wananchi waliofika uwanja ambao aliapishwa.


Wananchi wakiwa na mabango ya kumpongeza Rais Mnangagwa.

 Zimbabwe imempata rais mpya, Emmerson Mnangagwa, ambaye ameapishwa rasmi kuchukua wadhifa huo kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka 37 tangu lijipatie uhuru kutoka wa Waingereza.

Kifuatacho ni kiapo cha Emmerson Mnangagwa alichokitoa leo:

”Mimi Emmmerson Dambudzo Mnangagwa naapa kwamba kama Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe nitakuwa muaminifu kwa Zimbabwe na kuheshimu na kuilinda katiba pamoja na sheria zingine zote za Zimbabwe na nitalinda sheria zote zitakazoendeleza nchi hii na nitapinga chochote kitakachoiathiri Zimbabwe na nitalinda na kuimarisha haki za watu wa Zimbabwe na nitatekeleza majukumu yangu kwa nguvu zangu zote na uwezo wangu wote na nitaheshimu haki za Zimbabvwe na raia wake, ewe mwenyezi Mungu nisaidie”.

Upinzani unamtaka Mnangagwa, ambaye amekuwa mmoja wa watawala, kumaliza “utamaduni wa ufisadi”. Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 Jumanne iliyopita iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe.



Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo mjini katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa.

Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.

Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ataapishwa kaka uwanja michezo wa Harare.

Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang’atuke .

Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza “utamaduni wa ufisadi”. Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz