HII HAPA SIRI YA VIONGOZI VYAMA VYA UPINZANI KUHAMIA CCM - EDUSPORTSTZ

Latest

HII HAPA SIRI YA VIONGOZI VYAMA VYA UPINZANI KUHAMIA CCM


Image result for vyama vya siasa tanzania
IMEPITA miezi kadhaa tangu kuibuka kwa wimbi la wapinzani kurudi na wengine kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo gazeti hili limetonywa siri hasa za wanasiasa hao kufanya hivyo.


Ukiacha madiwani wa Arusha na Iringa, mapema wiki hii, CCM kilipokea ‘vigogo’ kadhaa kutoka Chadema na chama kichanga cha ACT-Wazalendo. Waliojiunga na CCM wakitokea Chadema ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha na Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi.

Waliojiunga na chama hicho wakitokea ACT-Wazalendo ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa chama hicho, Samson Mwigamba, Edna Sunga na wakili wa kujitegemea wa chama hicho, Alberto Msando.


Alberto Msando.

Kutoka CCM aliyeondoka na kujiunga na Chadema ni aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini,
Lazaro Samwel Nyalandu pekee na kuibua gumzo kubwa kutokana na ukubwa wa jina lake kisiasa.

Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya siasa za Bongo ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliyeomba hifadhi ya jina, kikubwa kinachofanyika ni ushawishi ili kukijenga chama sina uhakika nayo.

“Mbali na suala hilo, ukiwasikiliza wote wanaohamia CCM hawafichi kuwa wameguswa na utendaji wa Rais John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM.

“Wanadai wameguswa na mambo ambayo upinzani wamekuwa wakiyapigia kelele ya ufisadi, rushwa, kujilimbikizia kwani kuna walioamini kilikuwa kimepoteza mvuto, lakini sasa kina mguso kwa jamii. “Ukweli naomba nikiri kwamba kuna watu wanashawishiwa ili kukipa uhai chama.

Ndiyo maana kuwa wanaodaiwa wananunuliwa kama ilivyokuwa kwa wale madiwani wa Arusha, lakini hayo ya wengine ambao siyo madiwani kuhusu kupewa pesa ili wahame, mali na matumizi mabaya ya ofisi za umma ambayo sasa yanatekelezwa na Rais Magufuli.

“Wanasema hicho ndicho walichokitaka na kweli kinafanyika kwa vitendo. “Wengine kama Masha ndiyo wamekuja na hoja zao kwamba upinzani hauna nia ya kuchukua dola kwa kuwa chama mbadala, lakini hilo hakuliona ndani ya Chadema,” alisema mchambuzi huyo na kuongeza: “Dhana ya kuhama chama na kwenda chama kingine ni rahisi mno.

“Zipo sababu nyingine nyingi, lakini mtu anahama kwenda kwenye chama ambacho anavutiwa na sera ikijumuisha tunu, malengo, falsafa na itikadi zake.

“Katika jibu rahisi ni kwamba chama anachohamia mtu anaona kinakidhi matakwa yake ya kisera. Wapo wanaohama kwa sababu ya kukimbia migogoro. Wapo wanaokwenda kutafuta nyadhifa, wapo wanaokwenda kutafuta maslahi ya kifedha na vingine vingi sana hivyo ni lazima vyama viwe makini kwa watu wanaowapokea.”

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz