MCHORO WA YESU WAUZWA KWA MAMILIONI YA PESA - EDUSPORTSTZ

Latest

MCHORO WA YESU WAUZWA KWA MAMILIONI YA PESA


nMchoro wa Yesu Salvator Mundi au (Mkombozi wa Dunia) umeuzwa dola milioni 450 Marekani

Mchoro wa miaka 500 wa Yesu unaoaminiwa kuchorwa na Leonardo da Vinci, umeuzwa mjini New York kwa kima cha dola milioni 450.

Mchoro huo unajulikana kama Salvator Mundi (Mkombozi wa Dunia).

Ndio mchoro wa bei ya juu zaidi kuwai kuuzwa kwa mnada.

Leonardo da Vinci alifarika mwaka 1519 na kuna chini ya 20 ya michoro yake iliyobaki.

Ni huo mmoja tu unaoaminiwa kuwa mikononi mwa mtu ambao unaamimiwa kuwa ulichorwa baada ya mwaka 1505.Mchoro huo uliuzwa kwenye mnada

Picha hiyo inamuonyesh Yesu akiwa ameunua mkono mmoja huku mwingine ukishika kioo.

Mwaka 1958 mchoro huo uliuzwa kwenye soko la mnada mjini London kwa Dola 60. Wakati huo mchoro huo uliaminiwa kuwa kazi ya mfuasi wa Leonardo na wala haukuwa wa Leonardo mwenyewe.
Miaka minne iliyopita mchoro huo ulinunuliwa na raia wa Urusi kwa dola milion 127.5 lakini wakati huo hakuuzwa katika mnada.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz