DROO KOMBE LA DUNIA 2018 KUIFANYIKA URUSI - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 16 November 2017

DROO KOMBE LA DUNIA 2018 KUIFANYIKA URUSI


Droo ya Kombe la Dunia 2018 itafanyika ukumbi wa State Kremlin Palace

Baada ya mataifa 32 kufanikiwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Urusi, droo ya kupanga makundi ya timu hizo itafanyika kesho Ijumaa mjini Moscow.

Kuelekea zoezi hilo baadhi ya Timu ambazo zimepangwa chungu kimoja ni chungu cha kwanza ambacho kina timu mwenyeji Urusi, Ujerumani, Brazil, Ureno, Ajentina, Ubelgiji, Poland na Ufaransa.
Afrika inawakilishwa na Misri, Nigeria, Morocco, Tunisia na Senegal.

Na kuelekea fainali hizo FIFA wamesema mpaka sasa kuna maombi milioni 3.5 ya tiketi na walioomba wengi wao ni wenyeji Urusi.
Vyungu vimepangwa vipi?

Vyungu Kombe la Dunia
Chungu 1 Chungu 2 Chungu 3 Chungu 4
Urusi (wenyeji) Uhispania (8) Denmark (19) Serbia (38)
Ujerumani (1) Peru (10) Iceland (21) Nigeria (41)
Brazil (2) Uswizi (11) Costa Rica (22) Australia (43)
Ureno (3) England (12) Sweden (25) Japan (44)
Argentina (4) Colombia (13) Tunisia (28) Morocco (48)
Ubelgiji (5) Mexico (16) Misri (30) Panama (49)
Poland (6) Uruguay (17) Senegal (32) Korea Kusini (62)
Ufaransa (7) Croatia (18) Iran (34) Saudi Arabia (63)Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment