MCHEZAJI BORA SIMBA MWEZI WA OCTOBER ATANGAZWA - EDUSPORTSTZ

Latest

MCHEZAJI BORA SIMBA MWEZI WA OCTOBER ATANGAZWA

 MCHEZAJI BORA MWEZI OCTOBER
MCHEZAJI kiraka wa Simba, Erasto Nyoni ametangazwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo wa wa mwezi Oktoba.
Hiyo ni baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kwenye mechi nne za Ligi Kuu Bara ambacho amezicheza huku akisaidia timu yake kupata matokeo mazuri.


Kiraka huyo, alijiunga na Simba kwenye msimu huu wa ligi kuu akitokea Azam FC mara baada ya mkataba wake kumalizika.

Nyoni akicheza nafasi ya beki wa pembeni namba mbili hadi sasa tayari ameitengenezea mabao matano katika mechi za ligi ambazo amezicheza.


Erasto ambaye anamudu kucheza nafasi nyingi uwanjani amekuwa chachu ya matokeo mazuri kwa timu ya Simba tangu asajiliwe akitokea Azam FC.

Mechi ambazo zimempa uchezaji bora katika mwezi huu hadi kupelekea kutwaa tuzo hiyo ya uchezaji bora ni dhidi ya Njombe Mji, Stand United, Mtibwa Sugar na Yanga kati ya hizo walishinda mbili na kutoa sare mbili.
mwisho. like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz