LOWASSA: SINA MPANGO WA KURUDI CCM - EDUSPORTSTZ

Latest

LOWASSA: SINA MPANGO WA KURUDI CCM

Waziri mkuu huyo mstaafu amezungumzia kuhusu taarifa zinazoenea kuwa ameomba kurudi CCM.

Arusha. Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Lowassa amesema amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.

"Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM," amesema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema .

Amesema uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.

"Watu wanazuiwa kuja nyumbani kwangu, eti Serikali imezuia hivyo wanakuwa wanaogopa huu ni uongo Serikali haiwezi kuzuia watu kutembeleana," amesema.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz