MATOKEO YA MECHI YA TP MAZEMBE VS SUPER SPORT - EDUSPORTSTZ

Latest

MATOKEO YA MECHI YA TP MAZEMBE VS SUPER SPORT



Fainali ya kwanza ya mchezo wa shirikisho Africa imepigwa hii leo mjini Lubumbashi ambapo wenyeji Tp Mazembe wakiwa nyumbani waliikaribisha klabu ya Super Sport kutoka nchini Afrika Kusini.

Katika mchezo huo Tp Mazembe waliibuka kidede kwa ushindi wa bao mbili kwa moja ushindi ambao hauwapi uhakika kushinda kombe hilo baada ya mchezo wa pili utakaopigwa nchini Afrika Kusini.

Tp Mazembe walipata bao la kwanza dakika ya 18 ya mchezo huo kupitia kwa Adama Troure kabla ya Sipho Mbuli kuwapatia wageni bao la kusawazisha, dakika ya 68 ya mchezo Daniel Nii Adjei aliipatia Mazembe bao la ushindi.

Dakika 10 za mwisho za mchezo huo zilikuwa chungu sana kwa Super Sports kwani Tp Mazembe walihamia katika goli lao huku muamuzi wa mchezo huo akiwanyima penati baada ya Solomon Asante kuchezewa rafu katika eneo la box.

Mchezo wa marudiano utapigwa siku nane zijazo ambapo Super Sport watahitaji ushindi wa bao moja tu ili kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo huku Mazembe wakihitaji sare tu ili kutawazwa kuwa mabingwa. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz