REAL MADRID YAPIGWA 2-1 NA TIMU ILIYOPANDA DARAJA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 29 October 2017

REAL MADRID YAPIGWA 2-1 NA TIMU ILIYOPANDA DARAJA

Klabu ya Girona ilikataa katakata kuahirishwa kwa mchezo wao wa leo dhidi ya Real Madrid na waliahidi kwamba mchezo dhidi ya mabingwa hao wa Champions League itakuwa kama sherehe kwao.

Na Girona leo wamonesha kile ambacho kiliwafanya watamani kucheza dhidi ya Real Madrid baada ya kuwafunga Real Madrid kwa bao mbili kwa moja hii leo.

Ushindi wa leo wa Girona umesimamisha rekodi ya Real Madrid ya ushindi mara 13 mfululizo katika kiwanja cha ugenini na rekodi imekatwa na timu iliyopanda daraja.

Mara ya mwisho kwa Real Madrid kufungwa na timu iliyopanda daraja ilikuwa mwaka 2008 ambapo walifungwa na Almernia waliokuwa wametoka kupanda daraja.

Walianza Real Madrid dakika ya 12 kufunga kabla ya Cristian Stuan aliwafungia Girona bao la kusawazisha na kisha Cristian Portu akawafungia Girona bao la ushindi.

Kwa matokeo ya Real Madrid hii leo inawafanya pengo la alama kati yao na Barcelona kuongezeka na sasa Barcelona wanakaa kileleni wakiwa na alama 28, Valencia nafasi ya pili 24 na Real Madrid nafasi ya tatu 20.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment