MASHITAKA YA SIMBA WALIYOSHITAKI KWA DR MWAKYEMBE - EDUSPORTSTZ

Latest

MASHITAKA YA SIMBA WALIYOSHITAKI KWA DR MWAKYEMBE





Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema klabu yake imeandika barua kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe kumlalamikia baadhi ya matukio yanayozua utata yanayosababishwa na waamuzi wa ligi kuu Tanzania bara pindi Simba inapokuwa inacheza na timu nyingine.

Manara akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari amethibitisha kwamba, Simba imeandika barua kwenda TFF, Bodi ya Ligi, Chama cha Waamuzi na nakala imepelekwa kwa Waziri mwenye dhamana ya michezo (Dkt. Harisson Mwakyembe).

“Tumeandika barua TFF, Bodi ya Ligi na nakala tumempelekea Waziri mwenye dhamana ya Michezo na Chama cha Waamuzi, barua itakwenda kulalamikia maamuzi mabovu yanayofanywa na waamuzi wa mpira, sizungumzii Yanga ndio maana nimeweka matukio yote (Mbao na Stand) mechi zote zikiwa mfululizo”-Haji Manara.

“Niliwahi kushauri kwa TFF wakae na waamuzi wazungumze nao wawaeleze na sisi hatutaki kubebwa, tunataka ‘fair’ timu ikiwa inastahili kupewa penati dhidi yetu ipewa, tukistahili sisi tupewe. Goli halali likifungwa mwamuzi akubali.”

Manara analalamikia Simba kunyimwa penati kwenye mchezo dhidi ya Mbao uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza baada ya mshambuliaji wao John Bocco kuangushwa kwenye eneo la hatari (penati box) Manara pia amesema klabu yake ilinyimwa penati mbili wakati ilipocheza dhidi ya Yanga kufuatia Kelvin Yondani na Papy Tshishimbi kushika mpira kwenye eneo la hatari kwa nyakati tofauti.

Jambo jingine ambalo Manara amelipigia kelele kuhusiana na waamuzi ni klabu ya Stand kupewa penati isiyo halali kwa sababu mwamuzi alimtuhumu Ally Shomary kuushika mpira kwenye eneo la hatari lakini haikuwa hivyo.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz