KIKOSI CHA GUARDIOLA KINACHEZA SOKA MAALUM - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 31 October 2017

KIKOSI CHA GUARDIOLA KINACHEZA SOKA MAALUM


''Kikosi cha Guardiola kinacheza soka maalum''

Saa moja iliyopita

Sambaza habari hii Facebook
Sambaza habari hii Twitter
Sambaza habari hii Messenger
Sambaza habari hii Email
Mshirikishe mwenzako
nKikosi cha Guardiola kinacheza soka maalum, kulinagan ana kipa wa zamani wa ManCity

Pep Guardiola amebadilisha mchezo wa klabu ya Manchester City na sasa mchezo wa kikosi hicho umeanza kuwavutia mashabiki kote duniani kupitia ''soka maalum'' kulingana na kipa wa zamani wa klabu hiyo Shay Given.

Kikosi cha Guardiola kinaongoza ligi ya Uingereza kwa pointi tano kikiwa kimefunga mabao 35 katika mechi 10 na kupoteza pointi mbili pekee.

City ilimaliza katika nafasi ya tatu katika msimu wa kwanza chini ya ukufunzi wa raia huyo wa Uhispania na imetumia £200m kuwanunua wachezaji wapya msimu uliopita.

''Vipaji vilivyopo mbali na vile vilivyo miongoni mwa wachezaji wa ziada mara nyengine vinaziogopesha timu nyengine'', Given aliiambia BBCSport.

''Kikosi kilichoandaliwa na Guardiola kinavutia sana''.

''Amekuwa katika msimu wa kwanza na amekuwa akijifunza kuhusu kikosi chake na kukiimarisha''.

Ni vyema kuwa na vipaji , lakini la muhimu ni kuwapanga wachezaji hao na kuhakikisha kila mmoja wao anaonyesha umahiri wake na Guardiola nadhani amefanikiwa kutekeleza hilo.
 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment