YANGA KUMJARIBU AJIBU KWA PLUIJM LEO TAIFA - EDUSPORTSTZ

Latest

YANGA KUMJARIBU AJIBU KWA PLUIJM LEO TAIFA



Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi.

YANGA chini ya Kocha George Lwandamina, leo Jumamosi itacheza mechi ya kirafiki na Singida United inayonolewa na Hans van Der Pluijm kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kukijaribu kikosi chake chenye nyota kadhaa wapya akiwemo Ibrahim Ajibu.



Awali Yanga ikiwa kambini Morogoro hivi karibuni ilicheza mechi ya kirafiki na Moro Kids kwenye Uwanja wa Highland wa Chuo cha Biblia cha Baptist uliopo Bingwa, na Yanga kushinda mabao 5-0.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika kwa jumla kikosi chao kipo fiti kwa ajili ya pambano hilo.


Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu.

Saleh alisema, katika kikosi chao hakuna majeruhi baada ya beki wao wa pembeni, Hassan Kessy kupona maumivu ya nyama za paja na kuanza mazoezi Jumatatu asubuhi wiki hii.

“Kikosi kipo fiti na wachezaji wapo kwenye morali ya juu na tumetoka Morogoro leo (jana) asubuhi kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo huo na Singida.


Kocha wa Singida United, Hans van Der Pluijm.



“Kocha ataitumia mechi hiyo kwa ajili ya kuwaangalia wachezaji wapya na kikubwa anataka kutengeneza muungano mzuri kati ya hao wapya na zamani. Anataka kujua wamezoea kwa namna gani mfumo wake,” alisema Saleh.

Kwa upande wake, nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema; “Kambi ya wiki mbili imetujenga, mechi na Singida ni kipimo vizuri kwetu katika kujiandaa na msimu mpya.”

Kocha wa Singida, Pluijm alisema: “Nafurahia mechi hii ya kirafiki ambayo ni kipimo kwangu, kama unavyofahamu Yanga ni kubwa Afrika na Singida ni ndogo ambayo imepanda daraja.”


Wachezaji wa timu ya Singida wakiendelea na mechi.

Class alishinda pambano hilo lililofanyika mwezi uliopita nchini Ujerumani na taasisi hiyo imeamua kumfanyia sherehe ya kumpongeza kutokana na kutokea kwenye mikono yao. Sherehe hiyo itakayofanyika Bungoni, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mratibu wa sherehe hilo Habib Kinyogoli alisema kamati ya taasisi hiyo na makocha wa klabu za mchezo huo zimeamua kumpongeza bondia huyo kutokana na ubingwa wake kutambulika duniani.

“Tumepanga kumfanyia sherehe bondia Class, kesho Jumamosi (leo) kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata ya kushinda ubingwa wa GBC nchini Ujerumani mwezi uliopita.

“Sherehe hiyo itaambatana na uzinduzi mchezo wa ngumi kwa mabondia chipukizi kutoka katika klabu za mtaani ambao umebuniwa na KBF.

“Hii itajulikana kama kwa kifupi KMA ikiwa na maana ya Kila Mmoja Anaweza, mapambano hayo ya wazi yatasaidia kwa mabondia hao kujiandaa kuingia kwenye ngumi za kulipwa,” alisema Kinyogoli.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz